Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
🌎 Je, programu hii inategemea tovuti, vyanzo au "wasimamizi" wa nje ili kupakua machapisho, midia ya mkutano au maudhui mengine?
Hapana. Mfumo huu hufanya kazi kama tu JW Library. Inapakua machapisho, midia na maudhui mengine moja kwa moja kutoka kwa tovuti rasmi ya Mashahidi wa Yehova na mtandao wake wa utoaji midia. Programu huamua kiotomatiki kinachohitaji kupakuliwa na wakati midia iliyopakuliwa hapo awali si ya kisasa na inapaswa kupakuliwa tena.
Kidokezo
Code ya programu hii inapatikana kwa wote kuchunguza na kuthibitisha kinachoendelea chini ya maji.
🤔 Je, mfumo huu unakiuka sheria za utumiaji za tovuti rasmi ya Mashahidi wa Yehova?
Hapana. Sheria na Masharti ya tovuti rasmi ya Mashahidi wa Yehova huruhusu aina ya matumizi ambayo tunafanya. Hapa kuna nukuu kutoka kwa maneno hayo (msisitizo umeongezwa):
Haupaswi:
Kutengeneza programu za kompyuta, vifaa, au mbinu zenye kusudi la kukusanya, kunakili, kupakua, kupata (extract), kuvuna (harvest), au kutoa (scrape) habari (data), HTML, picha, au maandishi kutoka katika tovuti hii kwa kusudi la kusambaza. (Hii haitii ndani kusambaza programu za bure, zisizo za kibiashara zenye kusudi la kupakua faili za kielektoni kama vile, EPUB, PDF, MP3, AAC, MOBI, na faili za MP4 kutoka katika maeneo ya umma ya tovuti hii.)
☢️ Je, ninaripotije tatizo?
Tafadhali tuma suala kwenye hazina rasmi(repository) ya GitHub.
🆕 Ninawezaje kuomba kipengele kipya au uboreshaji?
Tafadhali fungua majadiliano kwenye hazina rasmi ya GitHub.
🤝 Ninawezaje kusaidia kwenye code?
Tafadhali angalia mwongozo wa kuchangia kwenye hazina rasmi ya GitHub.
❌ Je, ninaweza kutoa mchango kwa mradi?
Asante kwa nia yako ya kusaidia mradi! Hata hivyo, kwa kuzingatia Mathayo 10:8, michango haikubaliki na haitakubaliwa kamwe. Mfumo huu ulitengenezwa kwa upendo na wakati wetu wa ziada. Tafadhali furahia! 🎉
📖 Mathayo 10:8
"Mlipokea bure, toeni bure."