Kuhusu Meeting Media Manager (M³)
Programu hii ni nini?
Meeting Media Manager, au M³ kwa ufupi, ni mfumo kwa programu za Windows, macOS na Linux, ambayo hupakua kiotomatiki picha na video ambazo zitatumika kwenye mikutano ya kutaniko ya Mashahidi wa Yehova, kwa lugha yoyote kwenye tovuti rasmi ya Mashahidi wa Yehova.
Inaangazia usaidizi wa kudhibiti midia ya kawaida na midia maalum ya mikutano, na usaidizi kwa makutaniko mengi na/au vikundi vinavyotumia akaunti moja ya kompyuta.
Kidokezo
M³ ilikuwa ikijulikana kama JWMMF (JW Meeting Media Fetcher), lakini ilibadilishwa jina mnamo Mei 2022.
Mbona uchague M³?
M³ ni zana ya hali ya juu kwa wale wanaosimamia midia ya mkutano, ikiandaa utumiaji mkamilifu, unaotegemewa na wenye vipengele vingi kwenye mifumo mbalimbali.
Faida muhimu
Uwasilishaji wa media bila kuchoka: Kuwasilisha media kwa hali ya juu - fungua M³ na kila kitu kitafanya kazi. Hakuna kusanidi kugumu au hatua za ziada.
Unaweza kutumika na makutaniko mengi: Dhibiti mipangilio ya makutaniko au vikundi kadhaa kwa urahisi ndani ya programu moja.
Vipengele vya hali ya juu: Ongeza midia ya ziada, na pia shiriki kiotomatiki vyote vinavyoendelea katika Jumba La Ufalme na walio kwenye Zoom.
Utendaji ulioboreshwa kwa mifumo kadhaa: Furahia matumizi laini na yenye kutegemeka kwenye Windows, macOS na Linux, hata kwenye mifumo ya zamani au kompyuta zilizo na rasilimali chache.
Inategemewa na thabiti: Imeundwa ili kufanya kazi vyema unapoihitaji zaidi. Je, umekabili tatizo? Tafadhali ripoti, nayo itashughulikiwa ipasavyo.
M³ inaweza kukusaidia aje?
Kwa ufupi, M³ hukuruhusu kupakua, kusawazisha, kushiriki na kuwasilisha midia kwa urahisi na kiotomatiki.
Kwa mikutano ya zoom na ana kwa ana au ana kwa ana pekee, hali iliyojumuishwa ya uwasilishaji wa media ina vipengele vyote vinavyohitajika ili kurahisisha kazi ya kushiriki midia na kutaniko, ikiwamo:
- Vijipicha vya media vilivyo na uwezo wa kukuzwa na kugeuzwa, na pia kuweka nyakati maalum za kuchezwa na kusitishwa kwa midia
- Vitufe vya kusitisha/kucheza/kusimamisha vilivyo rahisi kutumia ili kudhibiti uchezaji wa faili za midia
- Uchezaji rahisi wa muziki wa usuli, na kusimama kiotomatiki kabla ya kuanza kwa mikutano iliyoratibiwa
- Utambuzi na usimamizi wa kiotomatiki wa scrini ya kando
- Kuwezeshwa kwa utumiaji wa OBS Studio pamoja na kubadilisha scene wakati wa kuwasilisha midia
- Kuwasilisha tovuti rasmi ya Mashahidi wa Yehova kwenye runinga nyingine
- Import JWPUB files, JWLPLAYLIST files and videos from the official website of Jehovah's Witnesses in a few clicks.
- Import Study Bible media and audio recordings of the New World Translation of the Bible in seconds.
- Always have a public talks media overview (S-34) one click away and ready to be used any minute you need it.
- Video maalum, picha, faili za sauti na hata faili za PDF zinaweza kuingizwa kwa urahisi pia!
Jaribu M³ leo na ujionee vile itakavyofanya kazi! Kuwasilisha midia kwenye mikutano ya kutaniko hakujawahi kuwa rahisi hivi.
Je, M³ inafanya kazi kwa lugha yangu?
Ndio! Midia kwa ajili ya mikutano ya Mashahidi wa Yehova inaweza kupakuliwa moja kwa moja kwa mamia ya lugha ambazo ziko kwenye tovuti rasmi ya Mashahidi wa Yehova. Orodha ya lugha zinazopatikana inasasishwa kwa ukawaida; unachohitaji kufanya ni kuchagua ni ipi unayohitaji.
Kwa kuongeza, M³ yenyewe imetafsiriwa katika lugha kadhaa na wajitoleaji wengi; kwa hivyo unaweza kusanidi lugha ambayo ungependa kuonyeshwa kwenye kiolesura/mwonekano wa M³.