Kutumia M³ kwenye Jumba la ufalme
Mwongozo huu utakuelekeza kwenye hatua za kupakua, kusakinisha na kuanzisha Meeting Media Manager (M³) kwenye Jumba La Ufalme. Fuata hatua ili kuhakikisha usanidi mzuri wa kusimamia midia wakati wa mikutano ya kutaniko.
1. Pakua na usakinishe
- Pakua aina ambayo inafaa mfumo wa kopyuta yako:
- Windows:
- Kwa mifumo mingi ya Windows, pakua meeting-media-manager-[VERSION]-x64.exe.
- Kwa mifumo ya kitambo ya 32-bit Windows, pakua meeting-media-manager-[VERSION]-ia32.exe.
- macOS:
- M-series (Apple Silicon): Pakua meeting-media-manager-[VERSION]-arm64.dmg.
- Intel-based Macs: Pakua meeting-media-manager-[VERSION]-x64.dmg.
- Linux:
- Windows:
- Ikiwa viunganishi vya kupakua havifanyi kazi, tembelea [Ukurasa wa kupakua wa M³] (https://github.com/sircharlo/meeting-media-manager/releases/latest) na upakue toleo ambayo inafaa.
- Fungua mfumo wa kupakua na ufuate maagizo ya kupakua M³ kwenye scrini.
- Fungua M³.
- Pitia programu ya usanidi.
macOS only: Hatua za ziada za kusakinisha
Onyo
Sehemu hii inatumika tu kwa watumiaji wa macOS.
Kutokana na hatua za usalama za mfumo wa Apple, hatua za ziada zitahitajika ili kutumia programu M³ iliyopakuliwa kwenye mifumo za hivi karibuni za macOS.
Wasilisha amri hizi mbili kwenye Terminal, rekebisha njia ya M³ inavyohitajika:
codesign --force --deep --sign - "/Applications/Meeting Media Manager.app"
sudo xattr -r -d com.apple.quarantine "/Applications/Meeting Media Manager.app"
Onyo
Kama mtumiaji wa macOS, utahitaji kufuata hatua hizi kila saa utapakua au kusasisha M³.
Maelezo
Command ya kwanza inasaini code ya programu. Hii inahitajika ili kuzuia M³ kuonekana kama programu hatari iliyotoka kwa mtu asiyejulikana.
Command ya pili hutoa bendera ya quarantine kutoka kwa programu. Bendera hiyo hutumiwa kuonya watu kuhusu mifumo au programu ambazo huenda ni hatari ambazo zimepakuliwa kutoka kwa intaneti.
Njia mbadala
Ikiwa bado huwezi kuwasha M³ baada ya kuweka amri hizo mbili zilizo kwenye sehemu iliyopita, tafadhali jaribu:
- Kufungua mipangilio ya Privacy & Security kwenye mfumo wako wa macOS.
- Tafuta ingizo(entry) la M³ na ubofye kitufe Open Anyway.
- Kisha utaonywa tena, na kupewa ushauri wa "kutofungua hii isipokuwa una hakika kuwa imetoka kwa chanzo cha kuaminika." Bonyeza Open Anyway.
- Onyo lingine litaonekana, ambapo utahitaji kuthibitisha ili kuzindua programu.
- M³ sasa inapaswa kuzindua kwa mafanikio.
Ikiwa bado ukona tatizo hata baada ya kufuata hatua hizo, tafadhali fungua tatizo(issue) kwenye Github. Tutafanya yote tuwezayo kukusaidia.
macOS pekee: Kuwasha tena uwasilishaji wa tovuti baada ya kusakinisha
Onyo
Sehemu hii inatumika tu kwa watumiaji wa macOS.
Watumiaji kadhaa wa macOS wameripoti kwamba uwasilishaji wa midia haufanyi kazi tena baada ya kupakua visasisho kwenye M³.
Ikiwa kidirisha cha midia ni nyeusi unapowasilisha tovuti baada ya kusasisha M³, jaribu hatua zifuatazo:
- Kufungua mipangilio ya Privacy & Security kwenye mfumo wako wa macOS.
- Nenda kwenye Screen Recording.
- Chagua M³ kwenye orodha.
- Bonyeza kitufe cha
-
(minus) ili kuiondoa. - Bonyeza kitufe cha
+
(plus) na uchague M³ kutoka kwa folder ya Programu. - Unaweza ombwa kufungua M³ kwa upya ili mabadiliko yafanye kazi.
Baada ya hatua hizi, screen sharing inafaa kufanya kazi kama inavyotakikana.
Kidokezo
Unaweza kupuuza hatua hizi ikiwa haupangi kutumia kipengele cha kuwasilisha tovuti. Kwa upande mwingine, ikiwa unapanga kutumia kipengele cha uwasilishaji wa tovuti, inashauriwa kufuata hatua hizi baada ya kila sasisho ili kuhakikisha kuwa kipengele kinafanya kazi inavyotarajiwa.
2. Programu ya Usanidi
Lugha ya programu
Unapofungua M³ kwa mara ya kwanza, utaulizwa kuhusu lugha ya mfumo unaotaka. Chagua lugha ya mfumo unaotaka kutumia kwenye mfumo wa M³.
Kidokezo
Hii sio lazima iwe lugha sawa na ile ambayo M³ itapakua media. Lugha ya upakuaji wa media itasanidiwa katika hatua ya baadaye.
Aina ya profaili
Hatua inayo fuata ni ya kuchagua aina ya profaili. Kwa ajili ya matumizi katika Jumba la Ufalme, chagua Kawaida. Hili litapanga mipangilio mingi ya kawaida ya matumizi katika mikutano.
Onyo
Unafaa kuchagua Nyingine ikiwa unatengeneza profile ambayo midia haifai kupakuliwa moja kwa moja. Midia itafaa kupakuliwa kwa mkono kwa profile hii. Profile ya aina hii hutumiwa zaidi katika M³ wakati wa shule za kitheokrasi, makusanyiko mzunguko, makusanyiko ya eneo na matukio mengine maalum.
Profile ya Nyingine haitumiwi kwa mikutano ya kawaida. Kwa ajili ya matumizi ya mikutano ya kutaniko, tafadhali chagua Kawaida.
Utafutaji wa kiotomatiki wa kutaniko
M³ itajaribu kutafuta ratiba, lugha na jina rasmi la kutaniko lako.
Ili kufanya hivyo, tumia kitufe cha Tafuta Kutaniko kando ya nafasi ya jina la kutaniko na ingiza angalau sehemu ya jina na mji wa kutaniko lako.
Kutaniko sahihi litakapo patikana na kuchaguliwa, M³ itajaribu kujaza habari nyingi iwezekanavyo, kama jina la kutaniko, lugha ya mikutano, na siku na wakati wa mikutano.
Kidokezo
Mbinu hii hutumia habari kutoka kwa tovuti rasmi la Mashahidi wa Yehova.
Kuingiza habari ya kutaniko kwa mkono
Ikiwa mbinu ya kutafuta kutaniko haikupata kutaniko lako, unaweza kuingiza habari hizo zinazohitajika moja kwa moja. Programu itakuruhusu kukagua /au kuandika jina la kutaniko lako, lugha ya mkutano, na siku na nyakati za mikutano.
Kupakua na kuhifadhi video kutoka kitabu cha nyimbo
Pia utapewa uwezo wa kupakua video zote kutoka kwa kitabu cha wimbo. Chaguo hili hupakua mapema video zote za kitabu cha nyimbo, na hivyo kupunguza muda unaochukua ili kupakua midia kwa ajili ya mikutano katika siku zijazo.
- Faida: Midia ya mkutano itapatikana kwa haraka zaidi.
- Hasara: Kiwango cha nafasi inayotumiwa itaongezeka kwa kiwango kikubwa, huenda hata kwa 5GB.
Kidokezo
Ikiwa mfumo wenu kwenu Jumba La Ufalme una nafasi, tunashauri kwamba muwashe chaguo hili ili kufanya utumiaji uwe rahisi.
Kuunganisha kwa OBS Studio (Si Lazima)
Ikiwa Jumba lenu La Ufalme linatumia OBS Studio kwa ajili ya upeperushaji wa mikutano kwenye Zoom, M³ inaweza kuunganshwa na programu hiyo. Kwenye uratibu, unaweza kusanidi OBS Studio kwa kuingiza yafuatayo:
- Port: Nambari ya Port hutumiwa kuunganisha mfumo na OBS Studio kupitia Websocket plugin.
- Password: Neno siri hutumiwa ili kuunganisha mfumo na OBS Studio kupitia Websocket plugin.
- Scenes: Scene za OBS itatumiwa wakati wa kuonyesha midia. Utahitaji scene moja inayoonyesha scrini ya midia, na moja inayoonyesha jukwaa.
Kidokezo
Ikiwa kutaniko lako hufanya mikutano pamoja na zoom, inashauriwa muunganishe OBS Studio.
3. Furahia kutumia M³
Uratibu wa programu unapokamilika, M³ iko tayari kukusaidia kupanga na kuonyesha midia kwenye mikutano ya kutaniko. Furahia kutumia programu hii! 🎉